FAIDA ZA TIKITI MAJI.
Tikiti maji ni tunda ambalo
kisayansi hujulikana kama Citrullus
lanatus katika familia ya
Cucurbitaceae, ambalo mmea wake hutoa maua na humea kwa kutambaa. Mmea huu
ambao hutoa matunda makubwa yaliyo na umbo la tufe au yai, asili yake ni huko
kusini mwa Afrika.
Ushahidi wa kihistoria ulionyesha
kuwa mmea huu ulilimwa huko Misri tangu milenia ya pili BC, na katika karne ya
kumi AD mmea wa tikiti maji ulikuwa umesambaa huko bara Hindi hata Mashariki ya
mbali.Lakini hapo badae ulimaji
wake ulifika huko Ulaya ya kusini na kusambaa duniani kote.Tafiti nyingi zimekuwa zikifanyika kujaribu kuzalisha mbegu za tikiki zenye kukabiliana na magonjwa yashambuliayo mmea huu.
wake ulifika huko Ulaya ya kusini na kusambaa duniani kote.Tafiti nyingi zimekuwa zikifanyika kujaribu kuzalisha mbegu za tikiki zenye kukabiliana na magonjwa yashambuliayo mmea huu.
Ijapokuwa watu wengi huamini kuwa
tikiti maji ni tunda lililo na maji na sukari peke yake, lakini ukweli ni kuwa
tunda hili lina aina nyingi ya virutubisho , mfano vitamini, madini na viondoa
sumu(antioxidants).
Jedwali likionyesha kiasi cha
virutubisho katika gramu 100 za tikiti maji.
Aina ya kirutubisho
|
Kirutubisho
|
Kiwango kilichopo
|
Vitamini
|
Vitamini A
|
28µg
|
Vitamini E
|
0.0 µg
|
|
Vitamini C
|
8.1mg
|
|
Thiamine
|
0.03mg
|
|
Niacini
|
0.2mg
|
|
Vitamini B 6
|
0.045mg
|
|
Folic acid
|
3mg
|
|
Madini
|
Kalshamu
|
7mg
|
Phosphorasi
|
11mg
|
|
Magnesiamu
|
10mg
|
|
Potasiamu
|
112mg
|
|
Munyu (Sodium)
|
1mg
|
|
Chuma
|
0.2
|
|
Zinki
|
0.1mg
|
|
Shaba
|
0.0mg
|
|
Manganizi
|
0.0mg
|
|
Protini muhimu
|
TRP(Tryptophan)
|
7.0mg
|
THR(Threonine)
|
27mg
|
|
ILE(Isoleucine)
|
19mg
|
|
LEU(Leucine)
|
18mg
|
|
LYS(Lysine)
|
62mg
|
|
MET(Methionine)
|
6mg
|
|
CYS(Cysteine)
|
2mg
|
|
PHE(Phenylalanine)
|
15mg
|
|
TYR(Tyrosine)
|
12mg
|
|
VAL(Valine)
|
16mg
|
|
ARG(Arginine)
|
59mg
|
|
HIS(Histidine)
|
6mg
|
Mbali na virutubisho
vilivyoonyeshwa katika jedwali, tunda hili la tikiti maji pia lina viondoa sumu
kama flavonoids, carotenoids na triterpenoids pia kiasi kikubwa cha
maji,na virutubisho hivi hulifanya tunda hili kuwa na sifa ya vyakula vyenye
faida kubwa mwilini.
Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa,
kuongeza matumizi ya vyakula vitokanavyo na mimea kama tikiti maji,matunda
mengine na mbogamboga hupunguza hatari ya kupata magonjwa, kuboresha maisha na
kuongeza umri wa kuishi. Twaweza kuepukana na magonjwa kama uzito mkubwa(obesity),kisukari na magonjwa ya moyo.
Ulaji wa vyakula hivi humfanya mtu kuwa na afya njema,ngozi yenye afya,nywele
na uzito ulio wa wastani.
Tunda hili lenye lycopene ambayo ni kiondoa sumu(antioxidant) na ambayo hulipa tunda hili
rangi ya kupendeza iliyo nyekundu au pink, pia hupatikana katika nyanya na
matunda mengine yaliyo na rangi nyekundu.
Tafiti za awali zimeonyesha kuwa
watu walao matunda kama tikiti na mengineyo yenye lycopene kwa wingi waweza kuwa na nafasi ndogo ya kupata maradhi
ya saratani hususani saratani ya tezi dume. Lakini hapajakuwepo kwa ushahidi
ulio thabiti kuonyesha uhusiano uliopo
kati ya saratani ya tezi dume na utumiaji wa matunda yenye lycopene ili kuweza kutambuliwa na mamlaka za chakula na tiba.
Katika utafiti mmoja
uliochapishwa mwaka 2013 katika jarida la
Kimarekani la shinikizo la damu, ulionyesha ulaji wa tikiti maji kwa watu
wazima walio na uzito mkubwa uliweza kupunguza shinikizo la damu la aota (aortic BP).
L-citrulline ni aina ya protini iliyo katika tikiti maji na ambayo
hubadilishwa mwilini katika figo na kuwa protini ijulikanayo kama L-arginine. L-citrulline pia huongeza utengenezwaji wa nitric oxide, ambayo hufanya mishipa ya damu kutokukakamaa na kuboresha
mzunguko wa damu mwilini na hii ndiyo sababu ya kupungua kwa shinikizo la damu.
Tunda hili limejipatia umaarufu kwa wale walio katika ndoa,kwa kuwa nitric oxide huongeza pia mzunguko wa
damu katika viungo vya uzazi, kwa hiyo wale walio na tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume kwa kiwango kidogo na kati, waweza kufaidika na tunda hili.
Kwa wana michezo ulaji wa tunda
hili au juisi yake ni wa faida kubwa kwa kuwa husaidia kupunguza maumivu ya misuli
na kuondokana na uchovu kwa haraka baada ya mazoezi au michezo ya kutumia
nguvu. Watafiti wanaamini kuwa hii ni kwa sababu ya uwepo wa protini ya L-citrulline katika tikiti maji.
Tikiti maji ni tunda muhimu
katika kurekebisha mmeng’enyo. Kwa kuwa
tunda hili limetengenezwa na kiasi kikubwa cha maji na fiba husaidia
kuondoa matatizo ya kukosa choo (constipation)
na kuboresha mmeng’enyo wa chakula tumboni. Pia kwa kuwa tunda hili lina
asilimia 92 ya maji na madini, huwa ni chaguo zuri kwa wagonjwa wenye upungufu
wa maji mwilini.
Hatari ya kupata ugonjwa wa pumu
ni mdogo kwa wale wanaokula aina fulani ya virutubisho. Katika moja ya
virutubisho hivi ni vitamini C ambayo hupatikana katika aina nyingi za matunda
na mbogamboga likiwemo tikiti maji.
Tikiti maji husaidia afya ya
ngozi kwa kuwa lina vitamini A na C. Vitamini A husaidia katika ukuaji wa tishu
za mwili,zikiwemo ngozi na nywele. Vitamini C husaidia katika utengenezaji wa
kolageni mwilini na husaidia kupona haraka kwa tishu zilizo na majeraha ikiwemo
ngozi.
Tahadhari
Tikiti maji siyo lishe
iliyokamilika peke yake, pia siyo tiba itakayokufanya kuacha kufuata ushauri wa
daktari. Ni vema basi kuhakikisha tunakula mlo ulio kamilika ili kujenga afya
bora. Tunapopata matatizo mbali mbali ya kiafya ni vizuri pia kuonana na
wataalamu wa afya kwa ajili ya utafiti, ushauri na kupata tiba iliyo sahihi.