UTANGULIZI
Viazi mviringo ni zao muhimu la
chakula na biashara katika nchi nyingi zilizoendelea na zinazoendelea. Viazi
husitawi vizuri sehemu za miinuko, kati ya meta 1300 na 2700 juu ya usawa wa bahari.
Hukomaa katika kipindi cha miezi mitatu hadi mitano. Viazi mviringo vina
asilimia kubwa ya chakula chenye asili ya wanga. Pia vina kiasi cha kutosha cha
protini, madini, vitamini na maji.
Mbegu
bora za viazi: Zinatakiwa kuwa na sifa zifuatazo
·
Zenye
kutoa mazao mengi zaidi kutoka kwenye shina moja
·
Ziwe
zimechipua vizuri na ziwe na machipukizi mengi (zaidi ya manne)
·
Zisiwe
na wadudu au magonjwa
·
Zitoke
kwenye aina ambayo haishambuliwi na magonjwa kama vile ugonjwa wa ukungu na
ugonjwa wa mnyauko bakteria
·
Zenye
ukubwa wa wastani (yaani zisiwe ndogo au kubwa sana) unaolingana na ukubwa wa
yai la kuku wa kienyeji
Aina bora za viazi
Taasisi ya
Utafiti wa Kilimo uyole, mpaka sasa imetoa aina sita za mbegu bora za viazi
mviringo nazo ni : Baraka, Sasamua, Tana, Subira (EAI 2329), Bulongwa [(K59a
(26)], Kikondo (CIP 720050)
Muda wa kupanda viazi: August hadi Septemba na Novemba hadi Decemba
Kupanda
Tumia sentimeta 60 (futi 2) hadi 75
(futi 2.5) kutoka mstari hadi mstari,
nafasi kati ya kiazi na kiazi iwe sentimeta 30
Mbolea
Ili kupata mazao mengi kutoka shambani
mkulima anashauriwa kutumia mbolea, aina ya
samadi, mboji, majani mabichi na za viwandani (au za chumvi chumvi).
Kwa
mbolea za viwandani tumia: Kilo 300 (au mifuko 6) ya mbolea ya TSP kwa hekta
moja, na kilo 300 (mifuko 6) za mbolea ya CAN au kilo 400 (mifuko 8) ya SA au
kilo 175 (mifuko 3.5) za Urea.
Palizi: Palilia viazi
wiki mbili au tatu baada ya kuchomoza. Inulia udongo ili kufanya tuta zuri ili
pawepo na unyevu wa kutosha na kufunika viazi kutokana na mwanga wa jua.
Magonjwa
na wadudu waharibifu:
Ili kuzuia ugonjwa wa ukungu tumia Ridomil. Changanya gramu 100 za dawa ya
Ridomil katika lita 20 za maji, na nyunyizia mara baada ya viazi kuchomoza na
baadaye kila baada ya wiki mbili au tatu kutegemea na hali ya hewa. Nyunyizia
dawa kama Karate kiasi cha mililita 20 mpaka 40 za dawa katika lita 20 za maji
ili kuzuia wadudu kama inzi weupe na wengineo. Tumia mbinu bora za kilimo kama
usafi wa shamba au kilimo mzunguko kama mbinu shirikishi katika kuzuia magonjwa
na wadudu.
Kuvuna
na mavuno:
Viazi huwa tayari kuvunwa baada ya miezi 3 hadi 5 kutoka kupanda. Muda wa
kuvuna utategemea madhumuni ya zao na aina iliyopandwa. Usiache viazi shambani bila kuvifunika (kwa
nyasi au udongo) kwa muda mrefu kwa sababu zifuatazo:
·
Viazi
vikipigwa na jua hubadilika rangi na kuwa na rangi ya kijani ambayo inavifanya
visifae kwa chakula.
·
Wadudu
kama vile nondo hutaga mayai juu yake, yanapoanguliwa viwavi hutoboa na kuingia
ndani ya viazi na kuviharibu
·
Iwapo
vitanyeshewa na mvua vitaharibika wakati wa kuvihifadhi ghalani.
Aina bora kama
Kikondo yaweza kutoa gunia 70 hadi
100 kwa ekari ikilimwa na kutunzwa vizuri.
Kuhifadhi: Viazi vya chakula vihifadhiwe kwenye
ghala yenye hewa ya kutosha, pasiwe na unyevu, joto kali. Unapohifadhi viazi
vya mbegu, aina mbalimbali zitengwe kwa kutumia vichanja au masanduku (maalum
ya kuhifadhia) tofauti.
0 comments:
Post a Comment