Tuesday, 31 January 2017
Saturday, 21 January 2017
HUYU SI MWANAMKE WA KUACHA
Mwanamke ambaye anakuwa na wasiwasi juu yako, anawaza kwaajili yako, hulia kwaajili yako, anajali hisia zako, hujishusha kwaajili yako na huweza kukuomba msamaha hata kama ni wewe umekosea ili tu kuleta amani si mwanamke wa kuacha.
Nimara chache sana kukutana na mwanamke kama huyu ambaye anaweza kujitoa kwaajili yako na kukuvumilia kwa wakati mgumu sana kwako. Wengi watapenda kukuona na kuwa na wewe katika kipindi cha mafanikio na mara nyingi hao ndipo ambao humfanya umsahau huyu.
Kwa bahati mbaya sana baadhi ya wanaume wakishavuka kwenye mitihani na kufanikiwa kidogo, huwasahau wale walioanza nao. Lakini baadaye huharibikiwa na kurudi kuomba msamaha, kabla hayajakufika yote hayo nikukumbushe tu kuwa wakati mwingine baraka ulizonazo si zako ni za mwanamke unayemdharau sasa.
Unaweza kumuondoa akaondoka na baraka zake ukajikuta unalia kulogwa kumbe mwenye baraka zake kaondoka. Hao wanaokuona wa maana leo ukiwa msafi ukikosa sabuni watakukimbia.
Mheshimu sana mwanamke aliyekuheshimu kabla hujaanza kujipulizia manukato kwani hao wanaokuzuzua leo siku wakisikia harufu ya jasho lako watakukimbia wakitapika. Precautions "it will comes back if it belongs to yu"
Wednesday, 18 January 2017
*UJUMBE MZURI KWA FAMILIA

*Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu. Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mmoja dhidi ya mwenzake. Tumevunjana moyo na kukatishana tamaa. Kwa hiyo, hakuna ndoa iliyokamilika wala familia iliyoboreka bila kuwa na mazoea au utamaduni wa kusameheana.*
*Msamaha ni nguzo au msingi wa utulivu wa akili na uhai wa roho zetu. Kama hakuna msamaha, familia inakuwa uwanja wa migogoro na mlipuko wa ugomvi. Panapokosekana msamaha, familia inaugua. Msamaha unahuisha moyo, kwa kusafisha fikra na kuufanya moyo kuwa huru. Binadamu asiyesamehe hana amani moyoni na wala hana urafiki au muunganiko na Mungu.*
*Maumivu ni sumu inayodhuru na kuua. Hebu kiponye kidonda hicho cha
moyo endapo kuna dalili za kujiumiza. Mtu asiyesamehe anajisababishia
mwenyewe ugonjwa wa mwili, kiakili na kiroho. Ndiyo maana familia
inapaswa kuwa sehemu ya uhai na si kifo; eneo la uponyaji na sio mahali
pa magonjwa; jukwaa la msamaha na si la uovu. Msamaha huleta furaha pale
uchungu ulipoleta maumivu; huleta uponyaji hata pale ambapo maumivu
yalisababisha magonjwa.*
```Ujumbe huu mzuri umfikie kila mmoja wetu katika familia yake. basi tuutafakari ujumbe huo```
```Ujumbe huu mzuri umfikie kila mmoja wetu katika familia yake. basi tuutafakari ujumbe huo```
Tuesday, 17 January 2017
Friday, 6 January 2017
KUTOKA JESHI LA POLICE:
KUTOKA JESHI LA POLICE:

USALAMA WA MAISHA YAKO.
* Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua. Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji. Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.
* Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige sehemu yoyote.
* Unapoiona line njiani ipo chini, usitake kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina shilingi ngapi ili uchukue salio. Simu inapoibiwa au
mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako, simu yako
inahusishwa na tukio hilo.
* Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa.
* Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina lako, hata kama baba yako, usikubali.
Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhu-miwa namba moja. Wengi wamepewa kesi za mauaji, wizi bila kujua. Polisi wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya.

USALAMA WA MAISHA YAKO.
* Usinunue simu za Android kwa mtu usiyemjua. Hiyo ni hatari kwani hujui huyo jamaa kaitoa wapi, mwisho wa siku unapewa kesi ya wizi au mauaji. Inawezekana simu hiyo iliibiwa kwa mtu aliyeuawa.
* Usimpe mtu usiyemjua simu yako apige sehemu yoyote.
* Unapoiona line njiani ipo chini, usitake kuiokota na kuiweka simuni mwako ujue ina shilingi ngapi ili uchukue salio. Simu inapoibiwa au
mwenye simu kuuawa, line hutupwa, unapoiweka simuni mwako, simu yako
inahusishwa na tukio hilo.
* Unapoweka salio, hakikisha karatasi ya vocha unaichana. Unapoitupa, watu wanaweza kufanya mauaji, wakachukua karatasi ya vocha ile na kuweka sehemu ya tukio au pale ulipoitupa kukatokea tukio na wewe kuhusishwa.
* Usikubali kumsajilia mtu line yake kwa jina lako, hata kama baba yako, usikubali.
Kumbuka namba yako umesajiliwa, moja ya matukio hayo yakitokea na namba yako kuonekana, moja kwa moja unakuwa mtuhu-miwa namba moja. Wengi wamepewa kesi za mauaji, wizi bila kujua. Polisi wapo kazini, wanapoona vidhibiti wanakuchukua kwani hawatojua kama umehusika au la. Kuweni makini ili usije kuingia matatizoni, simu yako, fedha zako, ukifanya kisicho sahihi kama uzembe, utaishia pabaya.
Monday, 12 December 2016
KWA NINI WATOTO HUPOTEZA HAMU YA KULA?
KWA NINI WATOTO HUPOTEZA HAMU YA KULA?
Kukosa
hamu ya kula ni tatizo la kawaida kwa watoto ambalo hupelekea wazazi
wengi kuwa na wasiwasi juu ya afya ya watoto wao.Kuna sababu nyingi
zinazoweza kusababisha kukosa hamu ya kula na tatizo hili
linapojitokeza tunatakiwa kuwa watulivu na kujaribu kuchunguza kwa
makini ni kwa nini mtoto anakosa hamu ya kula. Baadhi ya sababu zaweza
kutatuliwa na mzazi au mlezi lakini sababu nyingine kama zisababishwazo
na magonjwa zitahitaji msaada wa wataalam wa afya.
Moja ya sababu kubwa ambayo huwakosesha watoto hamu ya kula ni aina mbalimbali za magonjwa. Magonjwa kama
Malaria, kuhara, maumivu ya tumbo, maumivu ya kichwa,
magonjwa ya kinywa na koo, homa na mafua au dalili nyinginezo ambazo
humkosesha mtoto raha hupelekea watoto kukosa hamu ya kula.
Matatizo ya kifamilia na msongo ni sababu nyingine ambayo huwakosesha
watoto raha na hamu ya kula. Kama walivyo watu wazima watoto pia
hukumbana na matatizo ya kifamilia kama kupoteza ndugu au vitu
wavipendavyo. Lakini pia watoto hukumbana pia na changamoto mbalimbali
za kimaisha kama majukumu ya shule au pengine kukumbana na unyanyasaji
kama kuzomewa na mambo mengine mengi yanayokiuka haki zao. Kwa hiyo ili
kumuepusha mtoto na ukosefu wa hamu ya kula, wazazi na walezi hawana
budi kuwa makini endapo wataona mabadiliko yoyote ya kitabia ya mtoto.
Kugundua na kuweza kuziondoa sababu zinazomsababishia mtoto msongo,
tutaweza kuwarudisha katika hali ya kawaida na hamu ya kula itarejea
tena.
Lakini pia wakati mwingine hali hii hutokana na ugonjwa wa kukosa hamu ya kula ujulikanao kitaalam kama Anorexia nervosa.
Watoto wenye ugonjwa huu huweza kukaa muda mrefu bila kula ingawa
hawana tatizo jingine, na endapo watapewa chakula huchagua aina fulani
tu ya chakula jambo ambalo hupelekea kutopata mlo ulio kamili na hii
hupelekea kupungua uzito pamoja na kudhoofu kwa afya zao . Jambo hili
linapojitokeza ni vyema kumpeleka mtoto kwa wataalam wa afya wa masuala
ya lishe ambao watakuwa msaada mkubwa katika kumsaidia mtoto wako
kurejesha tena hamu ya kula.
Kiwango kidogo cha ukuaji wa mtoto huchangia kupungua kwa hamu ya kula.
Katika mwaka wa kwanza wa maisha ya watoto, watoto hukua haraka lakini
baada ya mwaka mmoja kiwango cha ukuaji hupungua na kiwango cha chakula
wanachokula pia hupungua.Katika wakati huo, hali hiyo ni ya kawaida
katika maisha ya watoto.
Sababu nyingine ambazo huchangia watoto kukosa hamu ya kula ni kama
maudhi ya dawa, upungufu wa damu, uambukizi wa minyoo na matatizo ya
mmeng'enyo mfano mtoto kutopata choo.
Maudhi ya dawa mbalimbali ambazo hutumika kutibu magonjwa kwa watoto
yanaweza kuchangia watoto kukosa hamu ya kula. Mfano daktari
akimwandikia mtoto dawa za antibiotiki, zaweza kusababisha tazizo la
kukosa hamu ya kula. Kupoteza hamu ya kula kwa watoto wanaotumia
antibiotiki ni maudhi ya dawa ambayo huwapata watoto wengi. Dawa
nyingine pia zaweza kupelekea kupata maudhi ya dawa kama kichefuchefu na
kutapika. Tatizo hili humalizika mtoto anapomaliza dawa na endapo
atakuwa amepona.
Uambukizi wa minyoo huchangia tatizo hili. Minyoo huingia katika mfumo
wa mmeng'enyo wa watoto na kusababisha upotevu wa damu. Minyoo hutegemea
ufyonzaji wa damu kama chakula chao, na katika uambukizi sugu hupelekea
kuvuja kwa damu,upungufu wa damu, kuhara,kichefuchefu,kutapika na
kukosa hamu ya kula. Endapo mtoto ataonyesha dalili za umbukizi wa
minyoo, ni vyema kuwaona wataalam wa afya ili kuweza kufanyiwa vipimo na
kupatiwa matibabu.
Ugonjwa wa upungufu wa damu ambao kwa kitaalam hujulikana kama anemia,
husababishia watoto tatizo hili. Kiwango kidogo cha madini ya chuma
katika damu, huwapata watoto ambao hawapati lishe ya kutosha yenye
madini haya. Lakini pia anemia yaweza kusababishwa na uambukizi
wa minyoo au hata magonjwa mengine. Watoto wenye anemia huwa wadhaifu na
wasio wachangamfu, na kama ugonjwa usipotibiwa utaathiri afya ya mtoto
hata maendeleo yake shuleni. Ni vyema mtoto akafanyiwa vipimo vya damu
endapo utahisi au ataonyesha dalili za ugonjwa wa anemia.
Kwa watoto hasa wadogo, kukosa choo hupelekea kukosa hamu ya kula. Kwa
hiyo inapotokea basi ni vyema kupata msaada wa wataalam ili mtoto aweze
kuondokana na tatizo hilo.
Wazazi na walezi wazingatie yafuatayo ili kuboresha hamu ya kula ya watoto wao:
- Kuwa na ratiba nzuri ya kumpa mtoto chakula, na mtoto apewa chakula anapokuwa na njaa.
- Usiwagombeze au kutoa maonyo makali kwa watoto wakati wa kula.
- Kuwa na milo midogo kati ya milo mikubwa.
- Mpe mtoto kiasi kidogo cha chakula lakini mara nyingi kwa siku na siyo kumshindilia kwa wakati mmoja.
- Usimlazimishe mtoto kula kama hana njaa.
- Hakisha mtoto anashiriki katika michezo, kwa kuwa michezo huusisha matumizi ya nishati ya mwili na kuboresha mifumo mbalimbali ya mwili.
- Wakati mwingine mpe nafasi mtoto wa uchaguzi wa chakula akipendacho, lakini chini ya uangalilizi wa mzazi au mlezi ili afanye uchaguzi ulio sahihi.
Wakati wote wazazi na walezi tukumbuke kuwa tatizo la kukosa hamu ya
kula ni la kawaida kwa watoto wengi, na tatizo linapojitokeza
hatuhitajiki kuwa na wasiwasi kila wakati. Kama mtoto wako ana afya
njema, anapata usingizi vizuri na ni mwenye furaha, hauna sababu ya kuwa
na wasiwasi. Lakini kama tatizo litaendelea kwa muda mrefu, basi hatuna
budi kuonana na wataalam wa afya kwa msaada zaidi.
FAIDA ZA TIKITI MAJI.
FAIDA ZA TIKITI MAJI.
Tikiti maji ni tunda ambalo
kisayansi hujulikana kama Citrullus
lanatus katika familia ya
Cucurbitaceae, ambalo mmea wake hutoa maua na humea kwa kutambaa. Mmea huu
ambao hutoa matunda makubwa yaliyo na umbo la tufe au yai, asili yake ni huko
kusini mwa Afrika.
Ushahidi wa kihistoria ulionyesha
kuwa mmea huu ulilimwa huko Misri tangu milenia ya pili BC, na katika karne ya
kumi AD mmea wa tikiti maji ulikuwa umesambaa huko bara Hindi hata Mashariki ya
mbali.Lakini hapo badae ulimaji
wake ulifika huko Ulaya ya kusini na kusambaa duniani kote.Tafiti nyingi zimekuwa zikifanyika kujaribu kuzalisha mbegu za tikiki zenye kukabiliana na magonjwa yashambuliayo mmea huu.
wake ulifika huko Ulaya ya kusini na kusambaa duniani kote.Tafiti nyingi zimekuwa zikifanyika kujaribu kuzalisha mbegu za tikiki zenye kukabiliana na magonjwa yashambuliayo mmea huu.
Ijapokuwa watu wengi huamini kuwa
tikiti maji ni tunda lililo na maji na sukari peke yake, lakini ukweli ni kuwa
tunda hili lina aina nyingi ya virutubisho , mfano vitamini, madini na viondoa
sumu(antioxidants).
Jedwali likionyesha kiasi cha
virutubisho katika gramu 100 za tikiti maji.
Aina ya kirutubisho
|
Kirutubisho
|
Kiwango kilichopo
|
Vitamini
|
Vitamini A
|
28µg
|
Vitamini E
|
0.0 µg
|
|
Vitamini C
|
8.1mg
|
|
Thiamine
|
0.03mg
|
|
Niacini
|
0.2mg
|
|
Vitamini B 6
|
0.045mg
|
|
Folic acid
|
3mg
|
|
Madini
|
Kalshamu
|
7mg
|
Phosphorasi
|
11mg
|
|
Magnesiamu
|
10mg
|
|
Potasiamu
|
112mg
|
|
Munyu (Sodium)
|
1mg
|
|
Chuma
|
0.2
|
|
Zinki
|
0.1mg
|
|
Shaba
|
0.0mg
|
|
Manganizi
|
0.0mg
|
|
Protini muhimu
|
TRP(Tryptophan)
|
7.0mg
|
THR(Threonine)
|
27mg
|
|
ILE(Isoleucine)
|
19mg
|
|
LEU(Leucine)
|
18mg
|
|
LYS(Lysine)
|
62mg
|
|
MET(Methionine)
|
6mg
|
|
CYS(Cysteine)
|
2mg
|
|
PHE(Phenylalanine)
|
15mg
|
|
TYR(Tyrosine)
|
12mg
|
|
VAL(Valine)
|
16mg
|
|
ARG(Arginine)
|
59mg
|
|
HIS(Histidine)
|
6mg
|
Mbali na virutubisho
vilivyoonyeshwa katika jedwali, tunda hili la tikiti maji pia lina viondoa sumu
kama flavonoids, carotenoids na triterpenoids pia kiasi kikubwa cha
maji,na virutubisho hivi hulifanya tunda hili kuwa na sifa ya vyakula vyenye
faida kubwa mwilini.
Tafiti nyingi zimeonyesha kuwa,
kuongeza matumizi ya vyakula vitokanavyo na mimea kama tikiti maji,matunda
mengine na mbogamboga hupunguza hatari ya kupata magonjwa, kuboresha maisha na
kuongeza umri wa kuishi. Twaweza kuepukana na magonjwa kama uzito mkubwa(obesity),kisukari na magonjwa ya moyo.
Ulaji wa vyakula hivi humfanya mtu kuwa na afya njema,ngozi yenye afya,nywele
na uzito ulio wa wastani.
Tunda hili lenye lycopene ambayo ni kiondoa sumu(antioxidant) na ambayo hulipa tunda hili
rangi ya kupendeza iliyo nyekundu au pink, pia hupatikana katika nyanya na
matunda mengine yaliyo na rangi nyekundu.
Tafiti za awali zimeonyesha kuwa
watu walao matunda kama tikiti na mengineyo yenye lycopene kwa wingi waweza kuwa na nafasi ndogo ya kupata maradhi
ya saratani hususani saratani ya tezi dume. Lakini hapajakuwepo kwa ushahidi
ulio thabiti kuonyesha uhusiano uliopo
kati ya saratani ya tezi dume na utumiaji wa matunda yenye lycopene ili kuweza kutambuliwa na mamlaka za chakula na tiba.
Katika utafiti mmoja
uliochapishwa mwaka 2013 katika jarida la
Kimarekani la shinikizo la damu, ulionyesha ulaji wa tikiti maji kwa watu
wazima walio na uzito mkubwa uliweza kupunguza shinikizo la damu la aota (aortic BP).
L-citrulline ni aina ya protini iliyo katika tikiti maji na ambayo
hubadilishwa mwilini katika figo na kuwa protini ijulikanayo kama L-arginine. L-citrulline pia huongeza utengenezwaji wa nitric oxide, ambayo hufanya mishipa ya damu kutokukakamaa na kuboresha
mzunguko wa damu mwilini na hii ndiyo sababu ya kupungua kwa shinikizo la damu.
Tunda hili limejipatia umaarufu kwa wale walio katika ndoa,kwa kuwa nitric oxide huongeza pia mzunguko wa
damu katika viungo vya uzazi, kwa hiyo wale walio na tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume kwa kiwango kidogo na kati, waweza kufaidika na tunda hili.
Kwa wana michezo ulaji wa tunda
hili au juisi yake ni wa faida kubwa kwa kuwa husaidia kupunguza maumivu ya misuli
na kuondokana na uchovu kwa haraka baada ya mazoezi au michezo ya kutumia
nguvu. Watafiti wanaamini kuwa hii ni kwa sababu ya uwepo wa protini ya L-citrulline katika tikiti maji.
Tikiti maji ni tunda muhimu
katika kurekebisha mmeng’enyo. Kwa kuwa
tunda hili limetengenezwa na kiasi kikubwa cha maji na fiba husaidia
kuondoa matatizo ya kukosa choo (constipation)
na kuboresha mmeng’enyo wa chakula tumboni. Pia kwa kuwa tunda hili lina
asilimia 92 ya maji na madini, huwa ni chaguo zuri kwa wagonjwa wenye upungufu
wa maji mwilini.
Hatari ya kupata ugonjwa wa pumu
ni mdogo kwa wale wanaokula aina fulani ya virutubisho. Katika moja ya
virutubisho hivi ni vitamini C ambayo hupatikana katika aina nyingi za matunda
na mbogamboga likiwemo tikiti maji.
Tikiti maji husaidia afya ya
ngozi kwa kuwa lina vitamini A na C. Vitamini A husaidia katika ukuaji wa tishu
za mwili,zikiwemo ngozi na nywele. Vitamini C husaidia katika utengenezaji wa
kolageni mwilini na husaidia kupona haraka kwa tishu zilizo na majeraha ikiwemo
ngozi.
Tahadhari
Tikiti maji siyo lishe
iliyokamilika peke yake, pia siyo tiba itakayokufanya kuacha kufuata ushauri wa
daktari. Ni vema basi kuhakikisha tunakula mlo ulio kamilika ili kujenga afya
bora. Tunapopata matatizo mbali mbali ya kiafya ni vizuri pia kuonana na
wataalamu wa afya kwa ajili ya utafiti, ushauri na kupata tiba iliyo sahihi.











