ManSillah

Tuesday, 1 November 2016

kilimo bora cha vitunguu

FAIDIKA NA KILIMO CHA VITUNGUU MAJI



UTANGULIZI

Vitunguu maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi
duniani zenye hali ya hewa ya ubaridi wastani. Zao hili lina wapatia
watu
shughuli za kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye
nyanja za uzalishaji hadi kwenye matumizi.

 Nchini Tanzania, vitunguu maji hulimwa kwenye mikoa ya

 Iringa wilaya ya Kilolo mpakani mwa mkoa wa Morogoro na kwenye maeneo ya mto Ruaha,

mkoani Arusha sehemu za Mang’ora na Babati,
 Kilimanjaro, na Morogoro wilayani Kilosa sehemu za Lumuma na Malolo na baadhi
ya sehemu za Mkoa wa Singida.


Hali ya Udongo

Vitunguu maji huhitaji udongo wenye rutuba, usiopasuka,
usiotuamisha maji na wenye mboji ya kutosha. Hali ya udongo katika
kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0.
Hali ya hewa
Hali ya hewa ifaayo ni ile ya ubaridi wastani. Joto linalohitajika ni
kati ya nyuzi joto 13 hadi 24°C ingawa kwa miche iliyoko kwenye
kitalu joto zuri ni la nyuzi 20 hadi 25°C. Joto la juu hufanikisha
utengenezaji wa kitunguu na ukaukaji.

Aina ya Vitunguu maji

Kuna aina nyingi ya vitunguu maji. Aina hizi zinaweza
kutofautishwa kulingana na:

(i) rangi ya ganda la nje la kitunguu kilichoishavunwa;

(ii) radha (utamu au ukali) wa kitunguu chenyewe;

(iii) mahitaji ya mwanga katika uzaaji: kuna aina yenye kuhitaji

siku fupi (mwanga wa saa 10 hadi 12 kwa siku) na aina
ihitajio siku ndefu (saa 13 hadi 14 za mwanga kwa siku) ili
kuweza kuweka kitunguu. Aina ya kwanza ndiyo ilimwayo
katika nchi za tropic.
Aina Siku za kukomaa  Umbile la kitunguu Rangi ya ganda Rangi ya ndani


1 Red Creole 


inakomaa kwa siku 150
umbile: Nusu bapa 
Rangi: Nyekundu, Nyekundu -
kahawia


Red Bombay


Inakomaa kwa siku 160
umbile: Duara Nyekundu
Rangi: angavu Nyeupe -kahawia


3. Texas Grano 

    Inakomaa kwa siku 165 
    Umbile: Duara Njano
     Rangi: (Kaki) Nyeupe

Uoteshaji miche na Upandaji

Vitunguu maji huoteshwa zaidi kwa kutumia mbegu kwenye kitalu
na kisha kupandikizwa shambani. Kiasi cha kilo 3.5 cha mbegu hutoa
miche ya kutosha kupandikiza eneo la hekta moja ya shamba.
Kusiha mbegu kwenye kitalu

Mbegu zinasiwa kwenye kitalu kilichoandaliwa vizuri. Mbegu
hupandwa kwenye kina cha sentimita moja kwa kumiminwa polepole
kwenye mistari/mifereji iliyoandaliwa vizuri. Kisha mbegu hufukiwa
kwa kunyunyizia udongo juu ya mbegu zilizoko kwenye mifereji.
Mbegu huota baada ya siku 7 hadi 10. Lakini hii hutegemeana na hali
ya hewa. Kwani mbegu huweza kuechelewa kuota hadi mpaka siku
21 udongo unapokuwa wa baridi. Hali ya hewa ikiwa nzuri, mbegu
uota mapema zaidi, hata ndani ya siku 4.

Kupandikiza vitunguu shambani

Miche hupandikizwa inapokuwa na urefu wa sentimita 15 na unene
1/2 au 3/4 ya penseli kwenye shina. Miche hii huwa imetimiza umri
kati ya wiki 7 hadi 9 kulingana na matunzo. Miche inapandikizwa
kwenye nafasi ya upana wa sentimita 20 hadi 30 na nafasi ndani ya
mstari ni sentimita 10 hadi 15.

Kuandaa shamba
Kabla ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe
kabisa. Kisha matuta au majaruba hutengenezwa ili kurahisisha
umwagiliaji.

Mbolea

Vitunguu maji vinamahitaji makubwa ya rutuba ya udongo. Hukua
vizuri vinapopata samadi ya kutosha kiasi cha tani 25 hadi 40. Kwa
hekta. Mbolea isambazwe shambani baada ya kupandikiza, lakini ni
vizuri zaidi kama ikichanganywa kwenye udongo kabla ya
kupandikiza. Kwa kuzingatia mazao ya tani 18 kwa hekta, vitunguu
huchukua kutoka katika udongo, kiasi cha wastani wa kilo 66, 11 na
70 za virutubisho aina ya Nitrojeni, Fosiforasi na Potasiam.
Hivyo kiasi cha mbolea kinachopendekezwa ni kilo 450 hadi 565 za
mbolea ya NPK (10-10-20) kwa hekta. Mbolea huwekwa siku 7 hadi
10 kabla ya kupandikiza. Kisha, inapendekezwa kuweka kiasi cha
kilo 13 hadi 18 za Nitrojeni baada ya wiki tatu hadi nne, ili kuongeza
ukuaji wa mimea. Upungufu wa kirutubisho cha Nitrojeni
unaharakisha ukomaaji na unapunguza ukubwa wa kitunguu.
Kirutubisho hiki kikizidi kupita kiasi huongeza ukubwa wa kitunguu
na unene wa shingo ya kitunguu, tabia ambayo upunguza ubora.

Umwagiliaji:

Umwagiliaji mzuri unahitajika ili kupata vitunguu bora. Umwagiliaji
wa maji yanayokwenda chini kiasi cha sentimeta moja au zaidi kwa
wiki ni mzuri kwa kupata vitunguu vikubwa. Epuka umwagiliaji
kupita kiasi au pungufu kwani hali hii huweza kusababisha
mipasuko.

Udhibiti wa magugu

Ukuaji na mavuno yanaathirika sana endapo magugu hayatadhibitiwa
mapema. Magugu yanadhibitiwa kwa kutumia madawa ama jembe
dogo la mkono. Wakati mwingine ni mchanganyiko wa madawa,
jembe la mkono na kungolea kwa mkono.
Udhibiti wa magonjwa

1. Ugonjwa wa doa la pinki (Purple blotch)

Uanza kama doa dogo linalozama ndani ya jani na kisha
linaongezeka ukubwa na kufanya rangi ya pinki. Kiini cha ugonjwa
huu huanzia kwenye mbegu na pia hubaki kwenye maozo ya majani
ya vitunguu. Aina ya Red Creole inaonyesha kutoshambuliwa sana
na ugonjwa huu.

Kuoza kwa kitunguu
Mbinu za kudhibiti ugonjwa huu ni kuendesha mzunguko (crop
rotation) wa muda mrefu wa mazao pamoja na kuzuia kutuama kwa
maji shambani. Kupunguza msongamano wa mazao shambani na
matumizi ya mbolea zenye calcium, phosphate and potassium
hupunguza kuenea kwa ugonjwa huu. Kwa upande mwingine,
matumizi ya mbolea ya nitrojeni kwa wingi au kwa kiasi pungufu
uongeza mlipuko wa magonjwa. Viatilifu kama vile Mancozeb
hutumika kuzuia mashmbulizi ya ugonjwa huu.

2. Ukungu wa unga (powdery mildew) na wa chini (Downy
mildew)


Magonjwa haya hushambulia majani ya mimea shamabani na hata
miche michanga. Kwenye majani kunaonekana vidoa vyeupe hasa
kwenye majani makuu ya mimea michanga. Ukungu mweupe
unatokea na kuongezeka kwa haraka kwenye sehemu au nyakati za
baridi. Viini huishi kwenye mabaki ya mimea ya vitunguu na huweza
kupeperushwa mbali na upepo. Kwenye mimea michanga ugonjwa
unaweza kudhibitiwa na madawa kama mancozeb.

3. Kuoza kwa vitunguu (bulb rots)

Hali hii inaweza kutokea shambani au wakati wa hifadhi ghalani.
Ugonjwa huu ni hatari zaidi kwenye sehemu za joto na zenye
kutuamisha maji. Ni vyema kuhakikisha kwamba shambani hakuna
hali ya kutuamisha maji na pia kwenye ghala kunakuwa na hali nzuri
ya mzuunguko wa hewa.

Udhibiti wa wadudu
Utitiri wa vitunguu (Onion thrips), Funza wa vitunguu (Onion
maggots) na Minyoo wa vitunguu (Onion wireworms) ni miongoni
mwa wadudu wasumbufu kwenye zao la kitunguu.

1. Utitiri wa vitunguu (Onion thrips)
Hawa ni wadudu wadogodogo sana ambao hula kwa kukwaruza juu
ya jani na kunyonya majimaji ya kwenye mmea. Hali husababisha
kutoka kwa mikwaruzo meupe kwenye majani ya vitunguu.
Mashambulizi yakizidi majani huanguka na kunyauka. Ukubwa wa
vitunguu hupungua. Hili ni tatizo kubwa zaidi hasa wakati wa ukame
kuliko wakati wa unyevu.
Utitiri wa vitunguu Madhara ya utitiri

2. Bungua weupe (White grub)
Huyu ni aina ya funza mkubwa. Hutaga mayai yake kwenye uozo wa
majani na samadi na hivyo mashamba ya vitunguu yaliyoko karibu
au kwenye maeneo ya jinsi hiyo huwa kwenye hatari zaidi.
Hushambulia mizizi na kusababisha kukauka kwa mimea. Kutifulia
shamba na kuwaweka wazi wadudu hawa kunapunguza idadi yao.

0 comments:

Post a Comment