Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo limepitisha Muswada wa sheria ya huduma za habari
(The Media Services Bill, 2016)
tayari kusainiwa na rais ili kuwa sheria kamili.
Muswada huo uliwasilishwa bungeni jana mjini Dodoma na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kisha wabunge wakaanza kuujadili. Muswada wa sheria ya huduma za habari wa mwaka 2016 umejadiliwa kwa siku mbili.
Jana Rais Magufuli wakati akifanya mahojiano na wahariri wa vyombo vya habari alisema ukifika mezani kwake hautafikisha dakika bila kusainiwa.
0 comments:
Post a Comment