ManSillah

Thursday, 3 November 2016

Shirikisho la vyuo Vikuu lataja Hujuma bodi ya Mikopo- (HESLB)

Shirikisho la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini limemuomba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufanya ukaguzi wa hesabu za Sh bilioni 1.74 za ada ya uombaji mikopo kwa mwaka huu katika Bodi ya Mikopo (HESLB) ili kujua matumizi ya fedha hizo kwa kuwa kuna mapungufu.

Aidha, shirikisho hilo limedai kubaini hujuma katika bodi hiyo zinazofanywa kwa makusudi ili kuchafua utendaji wa serikali iliyopo madarakani.

Hayo yalisemwa jana na Katibu Mtendaji wa shirikisho hilo, Daniel Zenda alipokuwa anazungumzia tuhuma za hujuma hizo, akidai zinafanywa kwa makusudi ili kurudisha nyuma jitihada njema za serikali.

Alisema ofisi ya CAG inapaswa kufanya ukaguzi wa Sh bilioni 1.74 fedha ambazo zilitokana na ada ya uombaji wa mikopo kwa mwaka huu ambapo kila mwanafunzi alitoa Sh 30,000 kwa waombaji 54,000.

Alisema ni muhimu kujua matumizi ya fedha hizo kutokana na upungufu uliojitokeza katika upitiaji wa sifa na vigezo vya wanaostahili kupata mkopo.

Alifafanua kuwa wanatambua hatua ya serikali katika kuhakikisha wanafunzi wenye sifa wanapata mikopo kwa wakati ambapo takribani Sh bilioni 80 zimeongezwa kwenye bajeti ya bodi hiyo ili kuwezesha mikopo kwa wanafunzi wote wenye sifa.

Zenda alisema Sh bilioni 487 zimepitishwa katika bajeti ya mwaka huu na mwaka jana ilikuwa chini ya makadirio ya Sh bilioni 350, lakini pamoja na kuongezeka kwa fedha hizo idadi ya wanafunzi walionufaika na mikopo imekuwa pungufu.

“Mwaka uliopita wanufaika wa mikopo walikuwa 53,000 na mwaka huu wanufaika wanafunzi 25,700 pamoja na ongezeko la makadirio ya zaidi ya Sh bilioni 137 kwenye bajeti ya Mikopo bado wanafunzi wengi hawajafikiwa,” alisema.

Related Posts:

  • USHAURI KWA VIJANA Ujumbe wa Leo:  1WaKorintho7:1-2 “Basi kwa habari ya mambo yale mliyoandika, ni heri mwanamume asimguse mwanamke. Lakini kwa sababu ya ZINAA kila mwanamume na awe na mke wake mwenyewe …..” TAFAKARI:   … Read More
  • KILIMO CHA VIAZI MVIRINGO UTANGULIZI Viazi mviringo ni zao muhimu la chakula na biashara katika nchi nyingi zilizoendelea na zinazoendelea. Viazi husitawi vizuri sehemu za miinuko, kati ya meta 1300 na 2700 juu ya usawa wa bahari. Hukomaa katika… Read More
  • ZISOME HIZI KUIMARISHA MAHUSIANO YAKO NA MWENZA WAKO Watu Wengi Ambao Wako Kwenye Uhusiano Wanalalamika Kuwa Wenzi Wao Hawawaoneshi Upendo Kama Ilivyokuwa Siku Za Mwanzo Za Uhusiano Wao. Wanaeleza Kuwa Wanaona Uhusiano Wao Unalegalega Na Mapenzi Yanapungua Taratibu Kama Bara… Read More
  • RAIS DKT MAGUFULI AMTEUA BW. CHARLES E. KICHERE KUWA NAIBU KAMISHNA MKUU WA TRA Read More
  • ni zao linalopendelea hali ya hewa ya joto na husitawi vema kati ya nyuzi joto 18°C hadi 35°C Udongo Hustawi vizuri katika udongo tifutifu wenye rutuba usiotuamisha maji Maandalizi ya shamba Lima shamba kwa trekta, kwa ng… Read More

0 comments:

Post a Comment