Mazoezi ni jambo muhimu sana kwa maisha ya wanaadamu wote katika k
ulinda afya za miili yao, watu wengi wamekuwa wakihangaika kufanya mazoezi kwa kuondokana na matatizo tofauti tofauti, wengine huenda wameshauriwa na Daktari kutokana na aina ya ugonjwa unaowasumbua na wengine hutaka kupunguza miili yao ili iwe katika muonekano mzuri na wengine wanataka kuilinda miili yao isije kunenepeana kiholela pia wengine hufanya mazoezi ikiwa ni sehemu ya utaratibu waliojiwekea katika maisha yao.
ulinda afya za miili yao, watu wengi wamekuwa wakihangaika kufanya mazoezi kwa kuondokana na matatizo tofauti tofauti, wengine huenda wameshauriwa na Daktari kutokana na aina ya ugonjwa unaowasumbua na wengine hutaka kupunguza miili yao ili iwe katika muonekano mzuri na wengine wanataka kuilinda miili yao isije kunenepeana kiholela pia wengine hufanya mazoezi ikiwa ni sehemu ya utaratibu waliojiwekea katika maisha yao.
Pengine
umejiuliza sana ni jinsi gani utafanya mazoezi kutokana na muda finyu
ulionao au mambo mbalimbali yanayopelekea usipate muda mwingi wa kufanya
mazoezi. Katika makala hii nakuletea aina 5 za mazoezi ambazo zinaweza
kukusaidia katika kuuweka sawa mwili wako na kuepukana na maradhi
mbalimbali.
1. KURUKA KAMBA
Pengine
unaweza kuona ni zoezi rahisi, lakini ni miongoni mwa mazoezi ambayo
yanasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza mafuta mwilini na kuunguza
calories nyingi kwa kila dakika utakayokuwa unaruka kamba. Zoezi hili
halihitaji uende Gym unaweza kuruka hata na watoto wako nyumbani mmoja
kashika huku na mwingine kule wewe unaingia kati unaruka, pia unaweza
kuruka peke yako.
2. KUPIGA PUSHAPU
Kwa
hali iliyozoeleka watu wengi wamekua wakikwepa kupiga pushapu kutokana
na ugumu mdogo unaoambatana na zoezi hili.lakini hili ni miongoni mwa
zoezi linaloweza kukuletea mabadiliko ya haraka zaidi katika mwili wako.
zoezi la pushapu ni zuri sana kwa kukuepushia maradhi ya moyo. huhitaji
kutumia nguvu sana kama unataka kupanda ulingoni ukapigane au utoke
misuli, ''Hapana'' piga pushapu chache kila asubuhi na jioni kwa kadri
ya uwezo wako hata kama ni 5 kwa asubuhi na 5 kwa jioni.
3. KUOGELEA
Hii ni
habari njema kwa wapenzi wa kuogele, ingawa kwa watanzania tulio wengi
tunachukulia kuogelea kama ni starehe tu na ni kitendo kinachopendwa na
watu wachache lakini ni miongoni mwa mazoezi yenye faida kubwa katika
mwili wa mwanadamu. Kuogelea kuna shusha blood pressure, kuimarisha moyo
na kuimarisha mfumo wa upumuaji. pia ni sehemu ya kufurahi na familia
yako ingawa kuogelea si zoezi rahisi kama kuruka kamba na pushapu.
4. KUKIMBIA
Kuna
manufaa mengi sana yanayopatikana kutokana na kukimbia, kwanza
hukuondolea misongo ya mawazo, inaimarisha afya ya moyo pia inaunguza
mafuta (calories) kwa kiasi kikubwa mwilini, kwa wale wenye miili minene
kukimbia ni moja ya mazoezi yanayo punguza mwili kwa haraka zaidi na
kutengeneza stamina kwa wanamichezo na hata wale wasiokuwa wanamichezo.
5. KUENDESHA BAISKELI
Wengi
wa watanzania hudhani kuendesha Baiskeli ni umasikini, kuingia kwa
bodaboda nchini kumepunguza kwa kiasi kikubwa waendesha baiskeli nchini,
watu wenye vipato kidogo hujisahau na kuishia kuendesha magari tu au
pikipiki na watu wa aina hii wana asilimia kubwa kuugua maradhi ya
kisukari na presha, Baiskeli itakufanya utumie nguvu nyingi ambazo zita
kuwa ni zoezi tosha katika kuupa mwili afya njema na kuepukana na
matatizo ya sukari na presha.
MWISHO ikumbukwe
kuwa pamoja na kufanya mazoezi pia unashauriwa kupangilia vizuri mlo
wako na si kufukia tu itakuwa unatia maji kwenye pakacha, hivyo basi ni
lazima uzingatie mlo sahihi kwa ajili ya afya yako.
0 comments:
Post a Comment