Saturday, 15 October 2016
Home »
» BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI YAHAMIA OFISI MPYA
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI YAHAMIA OFISI MPYA
HIGHER EDUCATION STUDENTS’ LOANS BOARD TUNAHAMA Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawajulisha wadau wake wote kuwa Ofisi yake ya Makao Makuu inahama kutoka Jengo la TIRDO, Barabara ya Kimweri, Msasani kwenda Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na. 46, Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge, Dar es Salaam kufikia Juni 30, 2013. Katika kipindi cha kuhama, Bodi itahakikisha huduma zinarejea katika hali ya kawaida ndani ya siku chache. Aidha uombaji wa mikopo kwa njia ta mtandao upo kama kawaida, na hivyo waombaji wa mikopo wanaweza kuendelea na utaratibu wa kuomba mikopo. Hata hivyo, huduma ya simu kwa waombaji wa mikopo imesitishwa kwa muda wakati mitambo ikifungwa na huduma itaendelea kama kawaida kuanzia Jumanne Juni 25, 2013 Bodi inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea wakati ikijiweka sawa katika makazi mapya. Imetolewa na: Mkurugenzi Mtendaji, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na.. 46, Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge S.L.P. 76068, Dar es Salaam, Tanzania. Simu: +255 22 2669036/2669037 Faksi: +255 22 2669039 Barua pepe: info@heslb.go.tz Tovuti : www.heslb.go.tz
Related Posts:
MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016 BOFYA HAPA KUANGALIA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2016… Read More
MATOKEO YA KIDATO CHA PILI 2016?17 BOFYA HAPA KUANGALIA … Read More
HUYU SI MWANAMKE WA KUACHA Mwanamke ambaye anakuwa na wasiwasi juu yako, anawaza kwaajili yako, hulia kwaajili yako, anajali hisia zako, hujishusha kwaajili yako na huweza kukuomba msamaha hata kama ni wewe umekosea ili tu kuleta amani si mwanamk… Read More
*UJUMBE MZURI KWA FAMILIA *Hakuna familia isiyo na mapungufu. Hatuna wazazi wasio na mapungufu, sisi pia si wakamilifu, hatuoi au kuolewa na mtu asiye na mapungufu, kadhalika watoto wetu nao si wakamilifu. Tunayo manung'uniko au malalamiko kila mm… Read More
AUDIO MPYA: NISHIKE MKONO kutoka kwa DAVID NYIGU | Download hapa Anafahamika kwa jina la DAVID NYIGU,ambaye anatamba kwa wimbo wake uitwao NISHIKE MKONO.. Ni wimbo mzuri kwa kweli na unao bariki sana.. Mwimbaji huyu anatokea Njombe ila kwa sasa anaishi Mbeya.... … Read More
0 comments:
Post a Comment