ManSillah

Sunday, 16 October 2016

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA KUJENGA TAIFA JKT LEO TAREHE 17.10.2016



  TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linapenda kuutaarifu umma juu ya utapeli unaoendelea kufanywa na baadhi ya watu wanaojifanya wanauwezo wa kuwaingiza vijana wa kitanzania kwenye mafunzo ya JKT kwa lengo la kupatiwa malipo.

Utapeli huo unafanyika kwa njia ya simu za mkononi kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno tofauti tofauti.

Jeshi la Kujenga Taifa linasisitiza kuwa ujumbe huo siyo sahihi na wananchi wanatakiwa kujiepusha na utapeli huo wenye lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Taarifa za mchakato wa uchukuaji wa vijana wa kujiunga na mafunzo ya JKT utolewa na Makao Makuu ya JKT kwa mfumo ulio rasmi wa mawasiliano ikiwemo luninga, radio, magazeti na tovuti ya JKT.

Aidha, JKT kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, inafuatilia kujua ni mtu gani au kikundi kipi kinahusika na utapeli huo ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa
Tarehe 17 Oktoba 2016

0 comments:

Post a Comment