ManSillah

Sunday, 30 October 2016

Bodi ya mikopo kufanya uhakiki wa wanafunzi













Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) imesema itaanza uhakiki wa
taarifa za wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo ili kujiridhisha kama wanasifa
sitahiki na ambao watakuta hawana sifa watasitishiwa mkopo.
Kwa ufupi
Mkurugenzi wa mtendaji wa HESLB, Abdul­ Razaq Badru amesema zoezi hilo litaanza Jumanne na wanafunzi wote watatakiwa kujaza dodoso ambalo litatolewa ambalo litawekwa kwenye mtandao wa bodi hiyo.

Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) imesema itaanza
uhakiki wa taarifa za wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo ili kujiridhisha kama
wanasifa sitahiki na ambao watakuta hawana sifa watasitishiwa mkopo.
Mkurugenzi wa mtendaji wa HESLB, Abdul­Razaq Badru amesema zoezi hilo litaanza Jumanne
na wanafunzi wote watatakiwa kujaza dodoso ambalo litatolewa ambalo litawekwa kwenye
mtandao wa bodi hiyo.
"Lengo letu ni kujiridhisha kama wanaonufaika wote kweli wanamahitaji sanjali na kuhakiki orodha yetu upya, katika hilo wale ambao hadhi zao zitaonesha kuwa sio wahitaji watapoteza sifa za kendelea kunufaika na mkopo," alisema Badru.

0 comments:

Post a Comment