ManSillah

TARUMBETA

Waungwana blogspot spousoured by Tarumbeta.

TARUMBETA

Waungwana blogspot spousoured by Tarumbeta.

TARUMBETA

Waungwana blogspot spousoured by Tarumbeta.

TARUMBETA

Waungwana blogspot spousoured by Tarumbeta.

TARUMBETA

Waungwana blogspot spousoured by Tarumbeta.

Monday, 31 October 2016

Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Yatoa Siku 90 Kwa Waliokosa Mikopo Kukata Rufaa


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza siku 90 kuanzia leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) kwa waombaji wa mikopo kwa mwaka wa masomo 2016/2017 kukata rufaa kwa njia ya mtandao ikiwa hawajaridhsihwa na matokeo ya upangaji uliotangazwa hivi karibuni.

Serikali imetenga Tshs 483 bilioni kwa ajili ya kutoa mikopo kwa jumla wanafunzi 119,012 – kati yao, wanafunzi 93,295 ni wanaondelea na masomo na wanafunzi 25,717 ni wa mwaka wa kwanza. Hadi sasa, jumla ya wanafunzi 20,183 wa mwaka wa kwanza wameshapata mikopo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo (Jumatatu, Oktoba 31, 2016) na Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru, Bodi imeanza kupokea rufaa hizo kwa njia ya mtandao (Online Loan Application and Management System) kuanzia leo (Oktoba 31, 2016) hadi Januari 31, 2017.

“Wanachotakiwa kufanya wanafunzi ni kuingia katika mtandao wetu wa http://olas.heslb.go.tz na kujaza fomu, kuichapa na kuiwasilisha kwa Afisa Mikopo wa chuo chake ambaye atawasilisha kwetu fomu zote za chuo chake kwa barua kwa ajili ya sisi kuzifanyia kazi,” amesema Bw. Badru.

ANGALIZO: Ada ya Maombi ya Tshs 10,000/- iliyopaswa kulipwa na waombaji mikopo kwa MPesa kwa ajili ya malipo ya Rufaa (HESLB) imefutwa.Taratibu nyingine zinabaki palepale

HESLB:APPEALS AGAINST MEANS TEST RESULTS FOR 2016/2017


The Higher Education Students’ Loans Board (HESLB) is hereby informing all loan applicants that the appeals window will be open for 90-days starting from 31st October, 2016. All Appellants should follow the below procedure: -
(i) You must complete the relevant Online Appeal Forms, make a printout of the same and attach thereto the necessary supporting documents.  The Online Appeals Form is accessible through http://olas.heslb.go.tz
  
(ii) After successful completion of the Online Appeal Form, the appellant must download the form and attach the necessary documents and hand over to the respective Higher Education Institution Loan Desk Officer.
(iii) Appeals must be routed through the respective Loan Desk Officers who will collect all appeal forms from their respective Institutions and submit them under covering letters to the Board.  The Board will not accept any appeal forms that will be submitted directly by students to the Board. 
(iv) The deadline for online submission of appeals will be 31st January, 2017.
ISSUED BY:
THE EXECUTIVE DIRECTOR
HIGHER EDUCATION STUDENTS’ LOANS BOARD
31st October 2016

Sunday, 30 October 2016

Basi likitokea Dodoma lagongana na Lori; magari yateketea kwa moto

Basi la Kampuni ya Safari njema lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea Dar es Salama. Limegongana na Lori katika eneo la Kimara Stopover.
Kuna ajali mbaya sana imetokea hapa eneo la Suca Mbele kidogo ya stop over ikihusisha lori na Basi T 990 ADF liitwalo Safari njema linalofanya safari zake kati ya Dar na Dodoma linaungua. SASA hivi yanaungua na watu waliokuwemo ndani.
FB_IMG_1477837647304.jpg

HESLB yafafanua vigezo utoaji mikopo, Waliokosa sababu zatajwa, wapewa nafasi ya kukata rufaa


Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Mikopo Bw. Abdul-Razaq Badru akifafanua jambo katika mkutano na wanahabari jijini Dar es Salaam leo (Jumapili, Oktoba 30, 2016). Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi hiyo Bw. Cosmas Mwaisobwa.

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa ufafanuzi kuhusu vigezo inavyotumia katika kuchambua, kupanga na kutoa mikopo kwa wanafunzi 20,183 (asilimia 74) wa mwaka wa kwanza hadi sasa kati ya 25,717 iliyopanga kuwapa mikopo katika mwaka huu wa masomo, 2016/2017.

Idadi iliyobaki (asilimia 26) ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza itajazwa na waombaji ambao baadhi ya nyaraka walizowasilisha zinaendelea kuchambuliwa ili kuthibitisha uhalisi wake na baadhi zitajazwa na waombaji ambao wanakata rufaa na kuwasilisha nyaraka zinazothibitisha uhitaji wao kwa mujibu wa vigezo vya mwaka huu.

Aidha, katika mwaka huu wa masomo, Serikali imepanga kutumia jumla ya Tshs 483 kutoa mikopo kwa wanafunzi 93,295 wanaoendelea na 25,717 wa mwaka wa kwanza.

Katika mkutano na waandishi wa habari leo (Jumapili, Oktoba 30, 2016), Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB Bw. Abdul-Razaq Badru amesema vigezo vikuu vinavyotumika mwongozo uliotangazwa na Bodi hiyo wakati ilipotangaza kuanza kupokea maombi mwezi Juni mwaka huu ambao unataja makundi makuu matatu ya watakaopata mikopo.

Vigezo vilivyotumika kutoa mikopo
Kwa mujibu wa Bw. Badru, kundi la kwanza linajumuisha wanafunzi waombaji wa mikopo wenye uhitaji maalum kama wenye ulemavu uliothibitishwa na Waganga Wakuu wa Wilaya na yatima ambao katika maombi yao waliwasilisha nakala za vyeti vya vifo zilizothibitishwa na makamishna wa viapo.

“Kundi la pili linajumuisha waombaji wa mikopo ambao baada ya uchambuzi wa taarifa zao walizowasilisha na baada ya kulinganisha na gharama za jumla za masomo yao ya sekondari, wamebainika kuwa wana uwezo mdogo wa kugharamia masomo yao ya elimu ya juu na hivyo kuwa na uhitaji zaidi wa mikopo,” amesema Bw. Badru.

Katika mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Bw. Badru ametaja kundi la tatu na la mwisho kuwa linajumuisha waombaji wa mikopo ambao wenye ufaulu wa juu katika matokeo yao ya kidato cha sita na wamechaguliwa kujiunga na fani za kipaumbele kwa taifa.

Fani hizo ni Sayansi za Tiba, Ualimu wa Sayansi na Hisabati, uhandisi wa Kilimo, Mafuta na Gesi na Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.

Makundi ya wanafunzi waliopata mikopo
“Hivyo basi, hadi sasa tumetoa mikopo kwa wanafunzi 20,183 wakiwemo wanafunzi yatima 4,321, wenye ulemavu 118, wanafunzi wenye uhitaji waliosomeshwa na taasisi mbalimbali katika masomo ya sekondari (87), wanafunzi wanaosoma kozi za kipaumbele 6,159 na wanafunzi wanaosoma kozi zisizo za kipaumbele lakini wanaotoka kwenye familia duni 9,498,” amefafanua Bw. Badru.

Sababu za kukosa mikopo
Katika mkutano huo, kiongozi huyo wa HESLB pia ameeleza kwa kina sababu nyingine za waombaji 27,053 ambao hawajapangiwa mikopo.

Ametaja sababu hizo kuwa ni pamoja na baadhi ya waombaji (90) kuwa na umri wa zaidi ya miaka 30, waombaji mikopo waliopata udahili kwa sifa linganishi (equivalent qualifications) na waombaji waliomaliza masomo ya kidato cha sita zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Kundi jingine la waombaji waliokosa mikopo katika awamu ya kwanza ni waombaji waliopata nafasi katika vyuo kwa ufaulu wa mitihani waliyofanya kama watahiniwa binafsi (Private Candidates) na waombaji ambao hawakurekebisha fomu zao za maombi ingawa waliitwa kufanya hivyo.

Nafasi ya rufaa na uhakiki wa wanafunzi wanaoendelea na masomo

Katika mkutano huo, Mkurugenzi Mtendaji huyo pia amewataka waombaji ambao hawajaridhika na upangaji wa mikopo unaotangazwa, kuwasilisha rufaa zao kwa njia ya mtandao utakaofunguliwa kuanzia katikati ya wiki ijayo.

“Tunafahamu kuwa kuna baadhi ya wanafunzi wamekosa mkopo kwa kutowasilisha baadhi ya nyaraka ingawa tuliwaomba kufanya hivyo, hawa na wengine wenye sababu za msingi, watapata fursa ya kuwasilisha rufaa zao kwa njia ya mtandao na nakala kuzituma kwa utaratibu tutakaoutangaza wiki inayoanza kesho,” amesema Bw. Badru.

Aidha, katika mkutano huo, Bw. Badru amesema bodi ya Mikopo inatarajia kuanza kazi kuhakiki taarifa za wanafunzi wanaoendelea na masomo ambao wanapata mikopo ya elimu ya juu kwa lengo la kubaini kama ni wana uhitaji wa mikopo hiyo kwa mujibu wa vigezo au hapana.

Katika zoezi hili linalotarajiwa kufanyika kwa siku 30 kuanzia mwezi ujao (Novemba, 2016), wanafunzi wote ambao ni wanufaika watalazimika kujaza dodoso maalum litakalokusanya tarifa za kiuchumi za wazazi na walezi wao ili kuweza kupata uhalisia wa sasa.

“Wanafunzi watakutana na dodoso katika akaunti zao katika mtandao wetu wa maombi ya mikopo (OLAMS) na watapaswa kujaza. Wale ambao hawatajaza dodoso hili kwa njia ya mtandao tutasitisha mikopo yao na wale ambao baada ya uchambuzi tutabaini hawana uhitaji, nao tutasitisha mikopo yao na watapaswa kuanza kurejesha fedha walizokopokea,’ amefafanua.

HESLB ilianzishwa mwaka 2004 na kuanza kazi rasmi mwezi Julai mwaka 2005 kwa lengo la kutoa mikopo kwa watanzania wahitaji waliopata nafasi za masomo katika vyuo vya elimu ya juu na kukusanya mikopo iliyoiva kutoka kwa wadaiwa walionufaika na mikopo tangu mwaka 1994.

NASAHA ZA BABA MWENYE BUSARA

Image result for african father
NASAHA ZA BABA MWENYE BUSARA
1. Mwanangu, mwanamke anaweza kuwa mkeo, mwingine anaweza kuwa
mama wa watoto wako, lakini ukipata mwanamke ambae atakuwa kama
mama kwako, mama kwa wanao na mama kwa familia, tafadhali mwanangu
usimuache huyo!
2. Mwanangu, usimfanye mwanamke wako kuwa ndio wa kupika na kufanya kazi zote za jikoni peke yake, tabia hiyo sio nzuri Kwani hata nyakati zetu, mashamba yetu yalijulikana kwa majina yetu wanaume lakini tulifanya kazi pamoja!
3. Mwanangu, nikikwambia wewe ni kichwa cha familia, simaanishi kutuna
kwa pochi lako, usiangalie kabisa pochi yako, angalia kama utaona tabasamu usoni kwa mke wako. Pesa sio kila kitu katika ndoa na haileti ukuu wa familia!
4. Mwanangu, ukitaka kuwa na maisha marefu na ukapunguza misongo ya
mawazo, ongea na mkeo pangeni bajeti ya mahitaji yenu, kisha mwache mkeo nawe na jukumu la kuratibu mahitaji ya kila siku ya familia kwa kumkabidhi fungu husika hata kama limetokana na michango yenu wawili. wanawake wanajua sana kupanga bajeti na hii haitakuwa rahisi kwa yeye kutumia hela hovyo wakati akijua kuwa nyumbani kuna mahitaji ya msingi,
lakini hela zikiwa mikono mwako ataendelea kuomba hata kama utakuwa
umeishiwa!
5. Mwanangu, Usithubutu kumpiga mkeo, maumivu ya kipigo hukaa ndani
ya moyo wake kwa muda mrefu sana na huacha kidonda ambacho hukawia sana kupona. Ni hatari sana kuishi na mwanamke mwenye majeraha moyoni!
6. Mwanangu, sasa unaamua kuoa,kama bado utaendelea kuishi maisha kama ya ubachela na mke wako, sio muda mrefu utakuwa bachela tena. ukioa Badilika anza kuishi maisha ya mke na mume!
7. Mwanangu, zamani,tulikuwa na wake wengi na watoto wengi kwa sababu
tulikuwa na mashamba makubwa na mavuno yalikuwa makubwa, lakini kwa
sasa maisha yamebadilika, kwa hiyo mkumbatie mwanamke wako peke yake kwani hakuna ardhi tena na mahitaji ya watoto ni makubwa sana. Angalia ukubwa wa familia yako!
8. Mwanangu, chini ya mwembe ambao nilikuwa nikikutana na mama yako
inaweza kuwa ni hoteli kubwa kwa nyakati zenu,lakini kumbuka, kitu pekee tulichoweza kufanya chini ya mwembe ilikuwa ni kukumbatiana pekee.nakushauri ukikutana na marafiki wa kike kikubwa unachoweza
kufanya nao ni kupeana mikono na ikizidi ni kukumbatiana hadharani sio
vinginevyo!
9. Mwanangu, usibadilike mara utakapoanza kupata mafanikio Zaidi, kuliko kuwahudumia hao viruka njia wa mtaani ambao hawajui mmetoka wapi na mkeo, nakushauri utumie na kufurahia mafanikio yako na mkeo ambae aliweza kusimama imara wakati wote wa mapito yenu magumu.
10. Mwanangu, kumbuka unapoanza kusema au kuona mke wako kabadilika, ujue kuwa kuna kitu ambacho ulikuwa ukikifanya umeacha kukifanya. Jitathmini na anza kufanya au kutimiza wajibu wako.
11. Mwanangu, usijaribu kumfananisha au kumlinganisha mke wako na
mwanamke mwingine wa nje, kwani hata yeye anakuvumilia sana na
hajakufafanisha na mwanaume mwingine yoyote huko nje na ndio
maana aliamua kuwa na wewe.
12. Mwanangu, sasa hivi kuna hiki kitu kinaitwa haki za wanawake, sawa,kama mwanamke anasema ana haki sawa na wewe katika nyumba, basi gawanya mahitaji yote ya ndani kwenu katika sehemu mbili zilizo sawa,halafu timiza nusu yako na mwambie atimize nusu iliyobaki.
13. Mwanangu, nilimuoa mama yako akiwa bado kigoli (bikira) na nilikuwa
naenda sana kwao kabla sijamuoa, lakini kutomkuta mkeo bikra kusikufanye umlaumu kuwa alikuwa muhuni, kumbuka wanawake wa enzi
zetu na wasasa ni tofauti, ulimchagua mwenyewe na ukigoli wake hukuujua
kabisa. Usiingize mambo ya kabla ya ndoa kwenye ndoa yenu.
14. Mwanangu, sikuwapeleka dada zako shule kwa kuwa nilikuwa mjinga
kama wazee wengi wa hapa kijijini wasemavyo, tafadhari usifanye ujinga
huu, kwani kiwango cha mafanikio ya wanawake sasa kimefanya wanaume
waonekane ni watu wa kawaida sana na sio muhimu kama enzi zetu.
Ukijaliwa watoto wape elimu.
15. Mwanangu, zamani enzi za ujana wetu, wanawake walikuwa na urembo
wa asili, ingawa siwezi kukudanganya, wengine waliongeza urembo kwa
kujichora hina na hata kutoboa pua na masikio lakini usisahau hawakuonyesha maumbile yao nyeti hadharani kama sasa. Hakikisha mkeo analijua hili!
16. Mwanangu, mama yako na mimi hatuna hisa katika kila kitu kinachoendelea kwenye maisha yenu, jaribuni kutatua changamoto zenu
wenyewe bila kila mara kuja kwetu kuomba usuluhishi. Ndoa ni pamoja na
ukomavu wa kutatua changamoto zenu bila kuziuza kama gazeti kwa kila mtu.
17. Mwanangu,nilimnunulia mama yako kifaa cha kupikia vitumbua ili
aanzishe mradi wa kuuza vitumbua, pia nilimsaidia kununua cherehani yake ya kwanza, tafadhari msaidie mke wako kutimiza ndoto zake kulingana na uwezo wako kama ambavyo unahangaika kutimiza ndoto zako.
18. Mwanangu, usiache kutusaidia mimi na mama yako, utu uzima una
changamoto nyingi sana na Mungu akikujalia utaziona muda ukifika.
Pamoja na kutimiza majukumu yako kama baba wa familia kumbuka pia
bado tunaishi na wewe ni mtoto wetu.
19. Mwanangu, kila upatapo muda wa kusali, Sali na familia yako, kuna kesho ambayo huijui, ongea na MUNGU wako ambae anajua kila kitu kila siku!
20.NAKUTAKIA MAISHA MEMA YA NDOA MWANANGU….NAKUPENDA!
SHARE NA MARAFIKI UPATE ZAWADI.

Bodi ya mikopo kufanya uhakiki wa wanafunzi













Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) imesema itaanza uhakiki wa
taarifa za wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo ili kujiridhisha kama wanasifa
sitahiki na ambao watakuta hawana sifa watasitishiwa mkopo.
Kwa ufupi
Mkurugenzi wa mtendaji wa HESLB, Abdul­ Razaq Badru amesema zoezi hilo litaanza Jumanne na wanafunzi wote watatakiwa kujaza dodoso ambalo litatolewa ambalo litawekwa kwenye mtandao wa bodi hiyo.

Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu(HESLB) imesema itaanza
uhakiki wa taarifa za wanafunzi wanufaika wanaoendelea na masomo ili kujiridhisha kama
wanasifa sitahiki na ambao watakuta hawana sifa watasitishiwa mkopo.
Mkurugenzi wa mtendaji wa HESLB, Abdul­Razaq Badru amesema zoezi hilo litaanza Jumanne
na wanafunzi wote watatakiwa kujaza dodoso ambalo litatolewa ambalo litawekwa kwenye
mtandao wa bodi hiyo.
"Lengo letu ni kujiridhisha kama wanaonufaika wote kweli wanamahitaji sanjali na kuhakiki orodha yetu upya, katika hilo wale ambao hadhi zao zitaonesha kuwa sio wahitaji watapoteza sifa za kendelea kunufaika na mkopo," alisema Badru.

Saturday, 29 October 2016

RAIS MAGUFULI ATENGUA UTEUZI WA MKURUGENZI WA MAKOSA YA JINAI TANZANIA

ANGALIA HAPA MATOKEO YA MTIHANI DARASA LA SABA 2016

Image result for necta
Serikali imetangaza matokeo ya mtihani wa darasa la 7 kwa mwaka 2016 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.52 na shule iliyoongoza kitaifa ni shule ya msingi Kwema ya mkoani Shinyanga.

Ufaulu wa mtihani wa Darasa la Saba umeongezeka kwa asilimia 2.52 kutoka asilimia 67.84 mwaka 2015 hadi kufikia asilimia 70.36 mwaka 2016.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Dk Charles Msonde ameyasema hayo leo wakati anatangaza matokeo ya mtihani wa taifa wa Darasa la Saba mwaka 2016.

Amesema, watahiniwa 555,291 kati ya 789,479 waliofanya mtihani huo mwaka huu wamefaulu na watajiunga na kidato cha kwanza 2017.

"Idadi hii ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 70.36, kati ya hao wasichana ni 283,751 na wavulana 271540. Mwaka 2015 watahiniwa waliofaulu ulikuwa ni asilimia 67.84 kuwa kuwapo ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.52,” amesema Dk Msonde.
 Watahiniwa 16,929 wamepata daraja A, 141,616 wamepata daraja B, watahiniwa 396,746 wamepata daraja C, watahiniwa 212,072 wakipata daraja D na 21,872 wakipata daraja E .

Aidha watahiniwa 238 wamefutiwa matokeo ya mtihani huo kutokana na udanganyifu. 
 

RAIS MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII


Rais Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza kwa kazi nzuri Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi baada ya kukagua pembe za ndovu 50 zilizokamatwa katika operesheni maalum ya kusaka majangili alipofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya Wizara ya Maliasili na Utalii (MPINGO HOUSE) jijini Dar es salaam leo Oktoba 29, 2016.


Wednesday, 26 October 2016

Monday, 24 October 2016

Audio | Q-boy ft Rayvanny & Shetta – MUGACHERERE | Mp3 Download

Audio | Q-boy ft Rayvanny & Shetta – MUGACHERERE | Mp3 Download 

Bonyeza hapa kudownload 

LIPUMBA AWATAKA CHADEMA KUTOINGILIA MGOGORO WA CUF

Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba,  amewataka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutoingilia mgogoro uliopo ndani ya chama hicho kwa sababu hauwahusu.

Kauli hiyo aliitoa jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na wanachama wa chama hicho katika kikao cha ndani, kilichofanyika Wilaya ya Kinondoni ambapo alisema Chadema kushindwa kutekeleza Operesheni Ukuta ni dhahiri chama hicho kimeshindwa kutekeleza kile wanachoahidi kwa Watanzania.

Alisema mpaka sasa kumekua na vikao mbalimbali vinavyofanywa na viongozi wa Chadema kwa ajili ya kuivuruga CUF, jambo ambalo alisema haliwekezani.

“Chadema wanajitahidi kutuvuruga kwa kutuma waasi wa chama hiki, lakini naomba niwaambie hawawezi, CUF ni ngangari hata serikali inajua na  wanachokifanya ni kupoteza muda bure.

“Unajenga Ukuta wa biskuti, ukiumwagia juisi unamong’onyoka, Ukuta gani huo, huu muziki wa CUF ni ngangari hawauwezi,” alisema Lipumba.

Alisema katika kipindi hiki ambacho wana kesi mahakamani, wanachama wa chama hicho wataendelea na shughuli za kukijenga chama hicho pamoja na kuwasisitiza  kuwa na msimamo wa kutetea chama na katiba yake, jambo ambalo linaweza kuwasaidia kufikia malengo waliyokusudia ya kushika dola kafika Uchaguzi wa mwaka 2020.

Alisema kutokana na hali hiyo, rasilimali za chama hicho zinasimamiwa kwa umakini chini ya walinzi wa chama hicho, Blue Guard ambao Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad alisema ni wavamizi hawatambui.

“Ninamshangaa Maalim Seif sasa hivi anaibuka na kusema hawatambui walinzi wa chama Blue Guard ambao miaka yote walikua wanamlinda pamoja na rasilimali za chama, lakini hayo yamekwisha nitazidi kumwomba aje tujenge chama hata kama kesi inaendelea mahakamani,” alisema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano anayemunga mkono Profesa Lipumba, Abdallah Kambaya alisema kupoteza nafasi ya umeya na naibu wake katika Manispaa ya Kinondoni ni matokeo ya mgogoro wa CUF na kutokuwepo ushirikiano ndani ya Ukawa.

“Maalim Seif anaunga mkono Ukawa, mbona wanachama wa Ukawa wameshindwa kutusaidia ili kupata meya na naibu wake kwenye uchaguzi wa leo? (jana),” alihoji.

Sunday, 23 October 2016

TCU inautangazia Umma kuwa itafungua Mfumo (CAS) kwa siku tatu tu, kuanzia Jumatatu tarehe 24 hadi Jumatano tare he 26 Oktoba 201

 
TAARIFA KWA UMMA
Tume ya vyuo Vikuu
Tanzania
(TCU) inautangazia Umma kuwa baada ya kukamilisha mchakato wa
maombi ya waombaji wa vyuo vikuu, vyuo Vikuu Vishiriki na Taasis
i za elimu ya juu kwa awamu ya
K
wanza
, ya
Pili
n
a ya
T
atu,
na matokeo ya waombaji wote waliofanikiwa kupata nafasi vyuoni
kukamilika, Tume ya vyuo Vikuu imebaini kuwa bado kuna waombaji takribani
5,301
ambao bado
wako kwenye mfumo na hawajakamilisha maombi yao.
Tume imebaini pia kuwepo kwa idadi kubwa y
a waombaji hasa wenye Stashahada ambao
hawakuomba kabisa kutokana na matokeo yao ya mi
tihani kuchelewa kufika Baraza l
a
Elimu ya
Ufundi (NACTE)
.
Awamu hii itawahusu:
Waombaji ambao bado wak
o ndani ya mfumo ambao hawajachaguliwa;
Waombaji wapya ambao hawaku
wahi kuomba awali; na
Waombaji walio na sifa linganifu ambao hawakukamilisha taratibu za uombaji hapo awali
Kuto
kana na sababu tajwa hapo juu, T
ume inautangazia Umma kuwa itafungua Mfumo (CAS)
kwa
siku tatu tu, kuanzia Jumatatu tarehe 24 hadi Jumatano tare
he 26 Oktoba 2016
ili kuruhusu
Makundi tajwa hapo juu kuingia kwenye mfumo kutuma maombi.
Waombaji wa
Awamu ya Nne
wanasisit
izwa kuzingatia yafuatayo:
Kuhakikisha wanaomba kozi walizo na sifa stahiki
Kuhakikisha wanakamilisha maombi yao kiufasaha
kuhakikis
ha wanajiridhisha na nafasi zilizopo kwa kuzingatia viwango vyao vya ufaulu.
Aidha Tume inapenda kuujulisha Umma kwamba kozi zote zisizo
onekana kwenye mfumo kwa sasa
kuwa zimejaa.
Baada ya tarehe tajwa hapo juu T
ume itafunga rasmi zoezi la udahili kwa mwak
a 2016/17 ili
kuruhusu mchakato mingine ya Bodi ya Mikopo na Vyuo kuendelea.
Kaimu Katibu Mtendaji
Tume ya Vyuo Vikuu
Tanzania 21/10/2016

WANAFUNZI FORM SIX WALIOPATA MKOPO CHUO KIKUU KCMC 2016/2017-BATCH 2

 WANAFUNZI FORM SIX WALIOPATA MKOPO CHUO KIKUU KCMC 2016/2017-BATCH 2



WANAFUNZI FORM SIX WALIOPATA MKOPO CHUO KIKUU KCMC 2016/2017-BATCH 2

VYUO VILIVYOTOA MAJINA YA WANUFAIKA WA MKOPO 2016/2017-AWAMU 1 & 2

 VYUO VILIVYOTOA MAJINA YA WANUFAIKA WA MKOPO 2016/2017-AWAMU 1 & 2
CHUO KIKUU KCMC 

CHUO CHA MAJI DSM  

CHUO KIKUU MUHAS  

CHUO KIKUU SUA  

CHUO KIKUU MUCE 

CHUO KIKUU DUCE  

CHUO KIKUU UDSM  


 

Bodi ya Mikopo Ya Elimu Ya Juu Zanzibar Yasitisha Kutoa Mikopo Kwa Wanafunzi Vyuo Vikuu

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein ameiagiza Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Zanzibar kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, kusimamisha utoaji wa mikopo ya elimu ya juu, hadi hapo serikali itakapojiridhisha na utaratibu mzima wa utoaji wa mikopo hiyo.

“Hatutatoa mikopo mwaka huu mpaka hapo tutakapokamilisha kazi ambayo tumeanza kuifanya ya kupitia upya utaratibu wa utoaji mikopo hiyo ili kuhakikisha inatolewa kulingana na mahitaji ya sasa ya nchi na kwa wanaostahili,” alisema Dk Shein.

Akizungumza katika hafla ya utoaji zawadi kwa wanafunzi waliofaulu daraja la kwanza katika mitihani ya Taifa ya Kidato cha Nne mwaka 2015 na Kidato cha Sita mwaka 2016, Dk Shein alisema kuwa katika utaratibu wa sasa wapo waliodanganya kupata mikopo na ambao wamekopeshwa lakini wamekuwa wagumu kurejesha mikopo hiyo.

Katika hafla hiyo, ambayo ilihudhuriwa pia na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Issa Haji Usii Gavu, jumla ya wanafunzi 119 waliomaliza kidato cha nne na wengine 50 waliomaliza kidato cha sita, walipewa zawadi kwa kupata daraja la kwanza katika mitihani yao ya taifa.

“Wako waliokejeli matokeo yenu, lakini ukweli ni huo mko 50 wa kidato cha tano mliopata daraja la kwanza na wengine 119 mliofaulu daraja la kwanza mtihani wa kidato cha nne,” alieleza Dk Shein na kuhoji msingi wa kukebehi matokeo hayo.

Aliongeza kuwa ufaulu wa wanafunzi hao, ni sifa kwa Zanzibar na anaamini kwa hatua zinazochukuliwa na serikali kuimarisha miundombinu ya elimu pamoja rasilimali watu kiwango cha ufaulu kitazidi kuongezeka.

“Mnapofanya mitihani sote tunakuwa na wasiwasi, nyinyi wenyewe, walimu, wazazi na sisi serikali kwa kuwa tunaelewa kuwa matokeo yoyote yale ni yetu sote kama ni mazuri ni furaha yetu sote na kama si mazuri ni huzuni yetu sote,” Dk Shein aliwaambia wanafunzi hao.

Dk Shein aliwataka wanafunzi hao kujivunia fursa waliyoipata na kuitumia vyema kujiimarisha kielimu, kwa kuwa haikuwa rahisi kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964 kuona vijana kutoka familia masikini wanapata fursa za kuingia sekondari kwa makundi.

“Mmepata bahati kubwa serikali yenu imeweka mazingira mazuri ya kupata elimu na haya ni matokeo ya utekelezaji wa ahadi ya Chama cha Afro-Shirazi na Rais wa Kwanza wa Zanzibar, Sheikh Abeid Amaan Karume ya kutoa elimu bure itakaposhika madaraka,” Dk Shein alieleza.

Katika hatua nyingine, Dk Shein ametoa wito kwa walimu wakuu kuhakikisha kuwa wanasimamia vizuri walimu katika shule zao pamoja na kuwahimiza wakaguzi wa shule kutimiza wajibu wao ipasavyo.

Dk Shein alisema; “kumekuwepo na tatizo la usimamizi maskulini, hivyo serikali itatengeneza utaratibu wa kuwapatia motisha walimu wakuu na wakaguzi watakaofanya vizuri kwa kuwa ni dhahiri kuwa walimu wakuu wakisimamia vyema skuli zao na wakaguzi wakaifanya kazi yao ya ukaguzi kwa umakini tutapata matokeo mazuri zaidi.”

Katika salamu zake hizo kwa wanafunzi hao, ambao walisindikizwa na uongozi wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali, pamoja na walimu wakuu wa baadhi ya shule, Dk Shein aliwataka walimu kuongeza ari ya kufundisha na kwamba ni heshima na furaha ya mwalimu kuona mwanafunzi wake anapata matokeo mazuri.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Mahira Baraka Hamadi wa kidato cha sita Skuli ya Biashara Mombasa Wilaya ya Magharibi Unguja akiwa ni mwanafuzi aliyefanya vizuri katika Mtihani wa Taifa Mei mwaka 2016,hafla iliyofanyika jana Ikulu Mjini Unguja

Thursday, 20 October 2016

HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI 1204 WALIOPATA MKOPO CHUO KIKUU SUA 2016/2017




 HAYA HAPA MAJINA YA WANAFUNZI 1204 WALIOPATA MKOPO CHUO KIKUU SUA 2016/2017
                    bonyeza hapa kuangalia

Wednesday, 19 October 2016

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU AJUCO SONGEA 2016/2017 AWAMU YA TATU

MAJINA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA CHUO KIKUU AJUCO SONGEA 2016/2017 AWAMU YA TATU

                BONYEZA HAPA KUANGALIA

Monday, 17 October 2016

New AUDIO | RAYVAN & NEY LEE - RUDI | Download

Sunday, 16 October 2016

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA JESHI LA KUJENGA TAIFA JKT LEO TAREHE 17.10.2016



  TAARIFA KWA UMMA
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) linapenda kuutaarifu umma juu ya utapeli unaoendelea kufanywa na baadhi ya watu wanaojifanya wanauwezo wa kuwaingiza vijana wa kitanzania kwenye mafunzo ya JKT kwa lengo la kupatiwa malipo.

Utapeli huo unafanyika kwa njia ya simu za mkononi kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno tofauti tofauti.

Jeshi la Kujenga Taifa linasisitiza kuwa ujumbe huo siyo sahihi na wananchi wanatakiwa kujiepusha na utapeli huo wenye lengo la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.

Taarifa za mchakato wa uchukuaji wa vijana wa kujiunga na mafunzo ya JKT utolewa na Makao Makuu ya JKT kwa mfumo ulio rasmi wa mawasiliano ikiwemo luninga, radio, magazeti na tovuti ya JKT.

Aidha, JKT kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, inafuatilia kujua ni mtu gani au kikundi kipi kinahusika na utapeli huo ili hatua kali za kisheria ziweze kuchukuliwa.


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Habari na Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa
Tarehe 17 Oktoba 2016

Saturday, 15 October 2016

Mwana Samatta kuwania Tuzo ya Mchezaji Bora ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania anayecheza soka la kulipwa katika klabu ya GENK ya nchini Ubelgiji ametajwa miongoni mwa wachezaji 30 wanaowani Tuzo ya Mchezaji Bora ya Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

Wachezaji wengine ni pamoja na Mkenya Victor Wanyama anayecheza ligi kuu ya Uingereza katika klabu ya Tottenham Hotspur, Denis Onyango kutoka Uganda anayekipiga katika klabu ya Mamelodi Sundowns.

Hapa chini ni orodha kamili.

1. Riyad Mahrez (Algeria & Leicester City)

2. El Arabi Hillel Soudani (Algeria & Dinamo Zagreb)

3. Islam Slimani (Algeria & Leicester City)

4. Samuel Eto’o (Cameroon & Antalyaspor)

5. Benjamin Mounkandjo (Cameroon & Lorient)

6. Serge Aurier (Cote d’Ivoire & PSG)

7. Eric Bailly (Cote d’Ivoire & Manchester City)

8. Yao Kouasi Gervais ‘Gervinho’ (Cote d’Ivoire & Hebei Fortune)

9. Mohamed Salah (Egypt & Roma)

10. Mohamed El Neny (Egypt & Arsenal)

11. Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Dortmund)

12. Andre Ayew (Ghana & West Ham)

13. Victor Wanyama (Kenya & Tottenham)

14. William Jebor (Liberia & Wydad Athletic Club)

15. Mehdi Benatia (Morocco & Juventus)

16. Hakim Ziyech (Morocco & Ajax)

17. John Mikel Obi (Nigeria & Chelsea)

18. Kelechi Iheanacho (Nigeria & Manchester City)

19. Ahmed Musa (Nigeria & Leicester City)

20. Cedric Bakambu (DR Congo & Villareal)

21. Yannick Bolasie (DR Congo & Everton)

22. Sadio Mane (Senegal & Liverpool)

23. Kalidou Koulibaly (Senegal & Napoli)

24. Keegan Dolly (South Africa & Mamelodi Sundowns)

25. Itumeleng Khune (South Africa & Kaizer Chiefs)

26. Mbwana Samatta (Tanzania & Genk)

27. Aymen Abdennour Tunisia & Valencia)

28. Wahbi Khazri (Tunisia & Sunderland)

29. Dennis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)

30. Khama Billiat (Zimbabwe & Mamelodi Sundowns

New AUDIO | Salamu TMK - Dada | Download

                                   Salamu TMK - Dada
                                          Download Here

BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI YAHAMIA OFISI MPYA


HIGHER EDUCATION STUDENTS’ LOANS BOARD TUNAHAMA Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawajulisha wadau wake wote kuwa Ofisi yake ya Makao Makuu inahama kutoka Jengo la TIRDO, Barabara ya Kimweri, Msasani kwenda Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na. 46, Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge, Dar es Salaam kufikia Juni 30, 2013. Katika kipindi cha kuhama, Bodi itahakikisha huduma zinarejea katika hali ya kawaida ndani ya siku chache. Aidha uombaji wa mikopo kwa njia ta mtandao upo kama kawaida, na hivyo waombaji wa mikopo wanaweza kuendelea na utaratibu wa kuomba mikopo. Hata hivyo, huduma ya simu kwa waombaji wa mikopo imesitishwa kwa muda wakati mitambo ikifungwa na huduma itaendelea kama kawaida kuanzia Jumanne Juni 25, 2013 Bodi inaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaotokea wakati ikijiweka sawa katika makazi mapya. Imetolewa na: Mkurugenzi Mtendaji, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, Kiwanja Na.. 8, Kitalu Na.. 46, Barabara ya Sam Nujoma, Mwenge S.L.P. 76068, Dar es Salaam, Tanzania. Simu: +255 22 2669036/2669037 Faksi: +255 22 2669039 Barua pepe: info@heslb.go.tz Tovuti : www.heslb.go.tz

SERIKALI YATANGAZA KIMA CHA CHINI MISHAHARA YA KISEKTA

Serikali imetangaza viwango vipya vya chini vya mishahara kisekta ambavyo vinatofautiana kati ya sekta moja na nyingine ambavyo ni kuanzia Sh40,000 hadi Sh400,000 kwa mwezi kuanzia Julai Mosi mwaka huu. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Wizara ya Kazi na Ajira, Ridhiwani Wema, watakaolipwa kima kidogo zaidi cha Sh40,000 ni wafanyakazi wa nyumbani ambao wameajiriwa na watu wa kawaida huku wakiishi kwenye nyumba za waajiri wao. Kwa upande mwingine, katika viwango hivyo, kima kikubwa katika viwango hivyo cha Sh400,000 kitalipwa kwa wafanyakazi wa sekta za mawasiliano zikiwamo kampuni za simu, kampuni za kimataifa za nishati, madini na taasisi za fedha. Katika viwango hivyo, mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na watu wa kawaida lakini ambao hawaishi kwenye nyumba za waajiri wao itakuwa Sh80,000. “Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na mabalozi wa kigeni na wafanyabiashara maarufu wanatakiwa kulipwa Sh150,000 kwa mwezi,” ilisema taarifa hiyo. Wafanyakazi wa nyumbani walioajiriwa na maofisa wa Serikali watalipwa Sh130,000 kwa mwezi. Kima cha chini cha mshahara katika huduma za kilimo ni Sh100,000 na huduma za afya Sh132,000. Kwa upande wa wafanyakazi wa vyombo vya habari, posta na usafirishaji wa vifurushi ‘courier services’, kima cha chini kitaanzia Sh150,000. Viwango vya chini vya mishahara kwa wafanyakazi wa hoteli za kitalii kuanzia Julai Mosi, mwaka huu ni Sh250,000, wakati kwa hoteli za kati ni Sh150,000 na migahawa, nyumba za wageni na baa ni Sh130,000. Kampuni za ulinzi za kimataifa zitapaswa kulipa kiwango cha chini cha mishahara cha Sh150,000 kwa wafanyakazi wake sawa na kampuni ndogo za huduma za nishati. Kampuni ndogo za ulinzi zitatakiwa kulipa Sh100,000. Kima cha chini kwa wafanyakazi wa sekta ya usafiri wa anga kitakuwa Sh300,000, sawa na wale wa utoaji na uingizaji wa mizigo. Wafanyakazi wanaofanya katika sekta ya usafirishaji wa majini, uvuvi na nchikavu wakitakiwa kulipwa Sh200,000. Kima cha chini kwa kampuni za makandarasi daraja la kwanza kitakuwa Sh325,000, makandarasi daraja la pili hadi la nne Sh280,000 na makandarasi daraja la tano hadi saba Sh250,000. Wafanyakazi katika kampuni za uuzaji wa magari watatakiwa kulipwa Sh300,000 na madalali wa bima watalipwa Sh200,000. Kampuni za wachimbaji wadogo wa madini zitalazimika kulipa mshahara usiopungua Sh200,000 kwa wafanyakazi wake. Mishahara ya chini kwa wafanyakazi wa shule za awali, msingi na sekondari za binafsi ni Sh140,000 huku wafanyakazi wa viwandani wakipaswa kulipwa Sh100,000. Taarifa hiyo ya Wizara ya Kazi imesema sekta ambazo hazijaorodheshwa, wafanyakazi wake watatakiwa kulipwa kuanzia Sh100,000.

BODI YA MIKOPO IMETANGAZA MAJINA 7904 YA WANAFUNZI WALIOPATA MKOPO 2016/2017

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imetangaza awamu ya kwanza ya majina ya wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu nchini watakaopewa mkopo kugharimia masomo yao.
 
Idadi ya wanafunzi ambao tayari wamepitishwa kupata mkopo ni 7,904, hata hiyo imeelezwa kiwango hicho kitaendelea kubadilika kwa kuwa mchakato unaendelea.

Taarifa iliyotolewa jana na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Stella Manyanya ilibainisha kuwa bodi imekamilisha uchambuzi wa majina ya waombaji ambao wana sifa zinazotakiwa na majina ya wanufaika wapya ambayo yameanza kutangazwa kupitia tovuti ya bodi hiyo.

 “Kwa kuzingatia mpango mkakati, pia mwongozo wa utoaji mikopo kwa mwaka 2016/17, Serikali imetoa vigezo vitakavyozingatiwa katika utoaji mikopo,” alisema Manyanya.

Alitaja vigezo vilivyotumika kuwa ni pamoja na vipaumbele vya kitaifa vinayoendana na mpango wa maendeleo wa Taifa wa miaka mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele.

Manyanya alizitaja fani zilizopewa vipaumbele kuwa ni sayansi za tiba na afya, ualimu wa sayansi na hisabati, uhandisi wa viwanda, kilimo, mifugo, mafuta na gesi asilia, sayansi asilia na mabadiliko ya tabianchi, sayansi za ardhi, usanifu majengo na miundombinu.

Katika taarifa yake, Manyanya alisema pia mchakato wa kuwapata wenye sifa za kukopa uliangalia uhitaji wa waombaji, hususan wenye mahitaji maalumu kama walemavu na yatima, ufaulu wa waombaji katika maeneo ya vipaumbele na umahiri. 
“Kuanzia mwaka huu wa masomo, wanufaika wote wa mikopo (wapya na wanaoendelea na masomo) watakopeshwa kulingana na uwezo wao katika vipengele vyote vya mikopo,” alisema.

Akizungumzia mchakato huo, mkurugenzi mtendaji wa bodi hiyo, Abdul Badru alisema unaendelea kufanywa kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa na timu ya bodi imejigawa katika vikundi ili kuhakikisha mipango inakwenda jinsi inavyotakiwa.

 “Timu ipo kazini na inafanya kazi yake kwa umakini. Kwa sasa majina ya waliochaguliwa kutokana na vigezo yamewekwa, lakini ni wahusika wenyewe au walezi na wazazi ndiyo wanaweza kuyaona kupitia namba zao za usajili wa kidato cha nne. Lakini siku chache zijazo tunaweza kuwataja wakaonekana kwa kila anayehitaji kuyaona,”